ACT Wazalendo yatangaza tarehe ya kuanza kampeni Jimbo la Dimani Zanzibar

474
0
Share:

Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Afisa Habari wake, Bw. Abdallah Khamis mapema leo kimetoa taarifa rasmi juu ya tarehe ya kuanza kampeni katika jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ilieleza: “Tunapenda kuwafahamisha wanachama wa ACT Wazalendo na umma wa watanzania kwa ujumla, kuwa kampeni  kwa ajili ya chama cha ACT Wazalendo katika jimbo la Dimani visiwani Zanzibar na kata mbali mbali kwa Tanzania bara ambazo chama kimesimamisha wagombea zitafunguliwa rasmi disemba 31/2016”

Aidha kiliongea kuwa, Kwa upande  wagombea Udiwani chama kilisimamisha wagombea saba na waliopitishwa na Tume ya uchaguzi ni wagombea sita baada ya mgombea wa Kata ya Misugusugu mkoani Pwani kuenguliwa kugombea kutokana na pingamizi alilowekewa.

Kata ambazo chama cha ACT Wazalendo imesimamisha wagombea ni pamoja na   Isagahe,iliyopo Kahama mkoani Shinyanga,Kijichi, iliyopo Temeke jijini Dar esSalaam, Nkome iliyopo Mkoani Geita,Tanga iliyopo mkoani Ruvuma na Ihumwa iliyopo mkoani Dodoma.

“Chama cha ACT wazalendo kina matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika maeneo tuliyosimamisha wagombea wetu na kuleta mabadiliko ya kiutendaji na kiuawajibikaji katika maeneo hayo huku tukitanguliza uzalendo kwa Taifa letu”.

Kwa kuimalisha Demokraasia Makini, Chama hicho kimewataka wanachama wake kuhakikisha wanaunga mkono mgombea wa upinzani mwenye kukubalika hasa pale tu ambapo hawakusimamisha mgombea. “Pale ambapo chama hakijasimamisha mgombea, wanachama, wafuasi na wapenda demokrasia na mabadiliko ya kweli tunawaomba wahakikishe wanamchagua mgombea wa upinzani ambaye ana nguvu katika eneo hilo. Tunawahimiza wanachama wetu na wapenzi wa demokrasia popote pale walipo katika kata zinazofanyika uchaguzi kuhakikisha wanaiondoa CCM  kwa kuwachagua wagombea wa vyama vya upinzani kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao” alimalizia  Afisa Habari huyo, Abdallah Khamis.

 

Share:

Leave a reply