ACT yaunga mkono sakata vyeti feki, yaitaka Serikali kujaza nafasi zilizowazi

404
0
Share:

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kinaunga mkono uamuzi wa Rais John Magufuli wa kufukuza kazi watumishi zaidi ya 9,000 waliogushi vyeti vya taaluma, kwa kuwa kitendo hicho kinashusha ufanisi wa kazi.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa ACT, Msafiri Mtemelwa ameitaka serikali kufanya hima kuzijaza nafasi za watumishi zilizo wazi  ili kutoathiri utolewaji wa huduma za kijamii hasa katika sekta ya afya.

“Sisi tunamuunga mkono Rais anapofanya vizuri sababu tunajenga nyumba moja, ingawa kuna baadhi ya mambo hatuyaungi mkono. Ila afanye him a kujaza nafasi zilizo wazi ili kutoathiri utolewaji wa huduma za kijamii,” amesema na kuongeza.

“Tunaunga mkono sababu watu hao wanashusha ufanisi wa kazi, kuna wasomi wengi hawana ajira, wawachukue wakafanye kazi.”

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply