Agizo la Makamu wa Rais wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu DSM

268
0
Share:

Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan amemtaka Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lazaro Mambosasa kuhakikisha kanda yake inatokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Mama Samia ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika Tamasha la 14 la Jinsia lililofanyika katika viwanja vya TGNP Mabibo.

“Bado takwimu za Jeshi la Polisi zinaonyesha ukatili wa kijinsia unaendelea. Kamanda Mambosasa tunakuachia wewe suala hili, likitokea tunakubana wewe na wewe utawabana wenzako,” amesema.

Mama Samia amesema serikali inaendelea kutekeleza Mpango mkakati wake wa miaka mitano wa kutokomeza ukatili wa jinsia ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto unapungua kwa asilimia 50.

Aidha, Mama Samia amewataka wanaume kutowanyanyasa wanawake kwa kuachana na mila na desturi potofu zinazokandamiza haki za wanawake na jinsia.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply