Agizo la Waziri wa Maji kwa Mhandishi wa Maji mkoa wa Mwanza

141
0
Share:

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng, Isaac Kamwele amemwagiza Mhandisi wa Maji Mkoa wa Mwanza kupeleka watalamu katika miradi ya maji iliyopo katika halmashauri ya Buchosa ilikubaini sababu zinazo pelekea miradi hiyo kuto kukamilika kwa wakati.

Eng. Kamwele ametoa agizo hilo baada ya kutembelea mradi wa maji wa luchili na Lumeya ambapo amebaini miradi hiyo hadi sasa imekwisha tumia  asilimia 5 ya fedha huku fedha zingine zikiwa hazijatumika.

Hata hivyo ameshangazwa na utata uliopo kwa halmashauri za Sengerema na Buchosa kushindwa kuweka wazi makabidhiano ya miradi hiyo  ambapo halmashauri ya buchosa imedai kuto  kabidhiwa miradi kutoka halmashauri ya Sengerema ili hali halmashauri ya Sengerema ikikili kukabidhi miradi hiyo katika halmashauri ya buchosa.

Awali akikagua miradi hiyo ameipongeza halmashauri ya Sengerema kwa kukamilisha mradi wa maji wa Nyamazugo kwa asilimia 100, ambapo amesema amefurahishwa na hatua hiyo kwani tayari wananchi wa Sengerema wananufaika na mradi huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Sengerema, Mac Agustine Makoye ameitaka serikali kuchukua hatua za haraka kubaini ugumu wa kuto kukabidhiana miradi kwa halmashauri hizo kwani kufanya hivyo ni kukwamisha ilani ya CCM ya mwaka 2015.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya Sengerema, Mwalimu Emmanuel Kipole amemhakikishia waziri wa maji kuhakikisha anachukua hatua kwa mkurugenzi atakaye baina kuidanganya ofisi ya mkuu wa wilaya, kuwa tayari makabidhiano yalishaa fanyika kwa halmashauri hizo

Share:

Leave a reply