Algeria kuipigania Morocco iwe mwenyeji wa Kombe la Dunia 2026

134
0
Share:

Serikali ya Algeria imetangaza kuunga mkono jitihada za Morocco kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.

Waziri wa Vijana na Michezo na Algeria, El Hadi Ould Ali amesema Rais Abdelaziz Bouteflika ndio amefanya maamuzi hayo ya kuinga mkono Morocco ili ipate nafasi hiyo ya kuwa mwenyeji.

Alisema iwapo Morocco itapata nafasi hiyo itakuwa fursa ya kipekee kwa namna moja au nyingine nchi hiyo na yenyewe itafaidika na uwepo wa mashindano hayo katika nchi jirani.

Nchi ambazo zinaomba kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mwaka 2026 ni Morocco, Canada, Mexico na Marekani na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) utachagua mwenyeji wa mwashindano hayo Juni 13 mwaka huu.

Iwapo Morocco itapata nafasi ya kuandaa mashindano hayo ya 23 itakuwa nchi ya pili barani Afrika kuapata nafasi hiyo baada ya Afrika Kusini ambayo ilikuwa mwenyeji mwaka 2010.

Share:

Leave a reply