Ali Kiba ajibu alichoimba Diamond Platnumz kwenye Fresh Remix

1677
0
Share:

Baada ya mwanamuziki Fid Q kutoa nyimbo ambayo amemshirikisha Diamond Platnumz ya Fresh Remix ambayo kuna baadhi ya maneno ameyaimba Diamond ambayo yanadaiwa kumhusu mwanamuziki mwenzake, Ali Kiba tayari yameanza kuibuka maneno mapya kuhusu wasainii hao wawili.

Katika wimbo huo wa Fresh Remix, Diamond amesikika akiimba,“Ukinichukia sikosi hela hivyo kwangu sio kesi , kunicompare na Cinderella aaah haiwezi kuwa fresh, Simba kutoka mbuga ya Tandale naona swala wanaforce tuwe salesale viuno vidogo wanataka ya pensi ya Pepe Kale si walitaka kiti nimewapa hadi itanda wakalale.”

Ali Kiba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika,“The KING ll always Be a KING. je Umeshakitandika nilale MALKIA wangu wa nguvu ?? #KingKiba” maneno ambayo yanatajwa moja kwa moja kumlenga Diamond Platnumz.

Share:

Leave a reply