Alichoandika mwanamuziki Tekno kwenye mtandao kwa lugha ya kiswahili

775
0
Share:

Lugha ya kiswahili ni wazi inazidi kuwa kubwa duniani kwa sehemu mbalimbali kuanza kuitumia na hata baadhi ya watu maarufu kujaribu kuzungumza ili tu na wao wawe kwenye listi ya watu ambao wanaweza kuzungumza kiswahili.

Star wa muziki kutoka Nigeria, Tekno amekuwa mmoja wa watu hao ambapo kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ujumbe kwa lugha ya kiswahili akielezea nyimbo yake mpya ya Samantha kuwa inapatikana kwenye mtandao wa kuuza nyimbo wa Wasafi.

Tekno ameandika,“Wanasema Utamu wa Ngoma uingie Ucheze….Haya watoto wazuri na wanangu wote wa Bongo Land ardhi ya Nyerere, twendeni tukaonje Huu Utamu Wa Pini yangu mpya ya kuitwa #SAMANTHA ila sio Mbwana….. ngoma iko Ndani Ya @wasafidotcom Kwa Mtonyo Wa Tsh 300 tu, Alafu Uje Unambie Umeionaje….Naskia eti Ngoma za Tekno hazijawai kumuacha mtu Salama?.….Haya twendeni tukaliamshe Dudeeeee!!!”

Share:

Leave a reply