Alichojibu Cristiano Ronaldo kuhusu mpango wa kuwa kocha baada ya kustaafu

661
0
Share:

Yawezekana imekuwa shauku ya watu wengi kusikia majibu ya staa wa Real Madrid ambaye ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia ya FIFA 2016 kuhusu kazi ambayo ataifanya baada ya kustaafu kucheza soka.

Cristiano Ronaldo amemaliza maswali ya watu wengi kwa kuweka wazi kuwa hana mpango wa kuwa kocha labda jambo hilo litokee kwa baadae lakini kwa sasa hajalifikiria.

“Ni ngumu sana, siwezi kujua nini kitatokea baadae lakini kwa sasa sijioni kama nitakuja kuwa kocha,” alisema Ronaldo wakati akifanya mahojiano na mtandao wa FIFA.

Kwa vipindi tofauti tofauti kumekuwepo na taarifa ambazo zimekuwa zikimshusha Ronaldo kuwa ataingia katika uigizaji baada ya kustaafu lakini likiwa ni jambo ambalo bado halijathibitishwa.

Share:

Leave a reply