Alichosema Shabani Kado baada ya kurejea Mtibwa Sugar

308
0
Share:
Goli kipa wa Timu ya Mtibwa Sugar, Shabani Kado ameeleza hali ya furaha kufuatiwa kurejea katika timu yake ya zamani yenye maskani yake Manungu Mkoani Morogoro
Kado,ambaye amerejeshwa hivi karibuni na kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mwadui ya Shinyanga amesema kwa sasa anajiskia vizuri kurejea timu yake ya zamani
“Kiukweli najiskia furaha kurudi katika timu yangu ya zamani na watu wategemee mambo mazuri tu,” alisema kado
Mlinda mlango huyo ambaye amerejeshwa baada wazee wa  Turiani hao kumuuza mlinda mlango wao bora wa Cosafa Said Nduda,ameendelea kuwa na imani juu ya timu yake kumaliza nafasi tano za juu kama ilivyokuwa msimu uliopita
“Mimi nafikiri suala la kumaliza nafasi za juu inategemea na ushirikiano mzuri katika timu kama timu ikiwa na ushirikiano mzuri basi tutamaliza nafasi za juu na kuleta mafanikio,” aliongeza Shabai Kado
Shabani kado aliwahi kuichezea Mtibwa Sugar kabla ya kuihama na kuelekea Mwadui ya Shinyanga,ambapo kufuatiwa wazee hao wa Manungu kumuuza Kipa wa Said Nduda kwenda simba,ikamrejesha chaguo lao la zamani Shabani Kado.
Na Rahimu Fadhili
Share:

Leave a reply