Alichosema Waziri Mahiga katika mkutano wa Baraza Kuu la UN

476
0
Share:

Katika kuhakikisha Tanzania inafikia malengo yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, serikali imesema imejipanga kuhakikisha kuwa inapunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini ambalo kwasasa linazidi kuwa kubwa kutokana na kuwepo na watu wengi ambao hawana ajira.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga wakati akihutubia katika mkutano wa 72 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambao unafanyika New York. Marekani.

Waziri Mahiga ambaye yupo katika mkutano huo akimwakilisha Rais Dk. John Pombe Magufuli alisema kuwa serikali kwasasa inatekeleza mipango mbalimbali ambayo itaiwezesha Tanzania kufikia malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati.

 

Aidha Waziri Mahiga alisema mwaka 2015 uchumi wa Tanzania ulikuwa kwa asilimia 7% kwa mwaka na unatarajiwa kukua kwa asilimia 10% ifikapo mwaka 2020 jambo ambalo litaiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.

Share:

Leave a reply