Aliyenusurika kifo auawa kwa kukatwa mapanga

329
0
Share:

Mlinzi mmoja wa maduka aliyenusurika kifo  kwa kukatwa katwa na mapanga katika kata ya Sima Wilayani Sengerema  mkoani Mwanza amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema. 

Kituo hiki kilifika katika hospitali hiyo alipokuwa amelazwa mlinzi huyo Charles  Guli mwenye umri wa miaka 55 makazi wa Ngara na kuzungumza na Mganga mkuu wa Hosipitali hiyo Dkt. Merry Joseph  ambapo alithibitisha kifo cha mlinzi huyo.   

Mlinzi Guli alifariki dunia huku mlinzi mwenzake Selemani Buyoga mwenye umri wa miaka  24 mkazi wa kitongoji cha Sima Majengo alifariki dunia kwa kukatwakatwa na mapanga  akiwa kazini.

Mwili wa marehemu  ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali  hiyo.

Tukio la kukatwa katwa kwa mapanga walinzi hao wa maduka katika kitongoji cha sima majengo Wilayani Sengerema limetokea mapema June, 8 mwaka huu.    

Kufuatia matukio haya ya walinzi kuuawa Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, Emmanuel    Kipole ameyatangazia vita makampuni yote ya Ulinzi Wilayani Sengerema yanayoajiri walinzi wasio na vigezo vya ulinzi .

Alisema kuwa serikali italifuatilia suala hilo na kwamba kampuni yoyote itakayokaidi zoezi hilo itachukuliwa hatua kali za kisheria .

Katika hatua nyingine Kipole alisema kuwa serikali inaendelea na uchunguzi wa watu wanaofanya  mauaji hayo ya walinzi kwani matukio hayo hayaipendezi kamwe serikali na jamii kwa ujumla.

 Na Veronica Martine, Sengerema

Share:

Leave a reply