Andres Iniesta afunga pingu za maisha kuichezea Barcelona

276
0
Share:

Nahodha wa Barcelona, Andres Iniesta amesaini mkataba mpya wa kuichezea Barcelona kwa miaka yote ambayo atakuwa akicheza soka.

Taarifa ya Iniesta kusaini mkataba wa maisha na Barcelona imetolewa na uongozi wa klabu hiyo, “Andres Iniesta amesaini mkataba wa maisha na Barcelona siku ya ijumaa, mkataba huo utamwezesha kuwepo katika klabu hii kwa muda wake wote ambao atakuwa akicheza soka.”

Iniesta alijiunga katika kituo cha kukuza vipaji cha Barcelona (La Masia) mwaka 1996 akiwa na miaka 12 na aliichezea timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002 na katika kipindi chote ambacho ameichezea Barcelona ameshinda makombe nane ya Ligi Kuu ya Hispania na makombe manne  ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Nahodha huyo wa Barcelona mwenye wa miaka 33 ameichezea Barcelona michezo 639 na kufunga magoli 55.

Share:

Leave a reply