Antoine Griezmann aeleza sababu ya kumwambia Ronaldo anamchukia

878
0
Share:

Siku kadhaa zilizopita staa wa Real Madrid, Cristiao Ronaldo alinikuliwa akisema kuwa mchezaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann alimwambia kuwa anamchukia katika mchezo ambao ulizikutanisha Atletico Madrid na Real Madrid.

Baada ya Ronaldo kusema maneno aliyoambiwa, Griezmann amefanya mahojiano na Jarida la L’Equipe na kuzungumza kuhusu maneno aliyomwambia Ronaldo kuwa hakuwa akimaanisha kweli na alichofanya ulikuwa utani wa kawaida.

Griezmann alisema hawezi kufanya hivyo kwani anamuheshimu Ronaldo na hata wakati wa mapumziko baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Ulaya walikutana Marekani na kupata nafasi ya kuzungumza.

“Nilikutana na Ronaldo akiwa na marafiki zake katika mgahawa Miami, nilikwenda kumsalimia na kumpongeza kwa Ureno kushinda kombe la Ulaya na yeyey kushinda Kombe la Klabu Bingwa Ulaya, tulifurahi pamoja,

“Nilimtania sababu nilitaka kuonekana mshindi baada ya mchezo kumalizika. Lakini kiukweli sio kwa sababu kanifunga katika michezo mwili mikubwa ya mashindano na kutufunga hat trick wikiendi iliyopita tulipokutana. Ninamuheshimu sana Ronaldo,” alisema Griezmann.

Share:

Leave a reply