Anusurika kuuawa kwa wizi wa mahindi wilayani Sengerema

693
0
Share:

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Paschal Mataba [14] mkazi wa Nyamazugo amenusurika kuuwawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kukutwa akiiba mahindi katika kitongoji cha kilabela kata ya mwabaluhi wilayani Sengerema.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa  kijtongoji hicho  Samweli Macheni Nzungu amesema tukio hilo limetokea mapema hii leo majira ya saa tatu asubuhi ambapo mwizi huyo amekutwa ndani ya nyumba ya James Lugodisha akiiba mahindi.                

Kwa upande wao wananchi wameomba kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kutoa taarifa kwa viongozi kwa mtu ambaye wanamtilia mashaka.

MO Blog imemtafuuta mtuhumiwa Paschal mataba amekiri kuiba mahindi hayo na kusema ni ugumu wa maisha hali ambayo   imepelekea kujiingiza katika wizi.

Hata Jeshi la polisi wilayani Sengerema linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa hatua zaidi.     

Na Emmanuel Twimanye, Sengerema

Share:

Leave a reply