Arsenal yakaribia kuipata saini ya beki Mustafi

271
0
Share:

Baada ya mabeki wa kati wa Arsenal wa kati, Per Mertesacker na Gabriek kupata majeraha, kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameingia sokoni kwa ajili ya kutafuta mchezaji mpya ambaye atakuja kucheza nafasi za wachezaji walio majeruhi.

Katika kutimiza azma yake, tayari inaripotiwa Arsenal ipo katika mazungumzo ya kukamilisha uhamisho wa beki wa Valencia, Shkodram Mustafi kwa kitita cha Pauni Milioni 30.

Mustafi, 24 ambaye ni raia wa Ujerumani kwa sasa yupo katika maandalizi ya msimu mpya na klabu yake ya Valencia na kama dili hilo litakamilika basi beki huyo wa zamani wa timu ya vijana ya Everton atajiunga na Arsenal.

Kwa upande wa Arsenal kwa sasa inafanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wake wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) dhidi ya Liverpool mchezo unaotaraji kupigwa Jumapili ya Agosti, 14 katika uwanja wa nyumbani wa Arsenal, Emirates.

Katika mchezo huo waa ufunguzi, Arsenal inataraji kumkosa beki wake Laurent Koscielny ambaye amerejea klabuni Jumatano na kocha Wenger anataraji kuwatumia mabeki wa timu ya vijana chini ya miaka 21, Culum Chambers na Rob Holding.

Share:

Leave a reply