Asya Idarous Khamsini kunogesha tamasha la Shikamoo Swahili Fest-Atlanta, GA leo

239
0
Share:

Mama wa Mitindo anayefanya vizuri ndani ya Tanzania na Nchini Marekani, Asya Idarous Khamsini jumamosi hii ya Oktoba 22 anatarajia kunogesha tamasha la Shikamoo Swahili Fest, Atlanta, GA ambapo tamasha hilo ni maalum kuenzi Kiswahili kama lugha ya Afrika Mashariki pamoja na tamaduni zake ambapo watu mbalimbali watajumuika pamoja.

Mwanamitindo Asya Idarous Khamsini anatarajia leo kuonyesha mavazi mbalimbali ya asili ya Tanzania na utamaduni wake na kubainisha kuwa yatakuwa chachu na mvuto kwa watu wote kwenye tukio hilo.

Pia kutakuwa na michezo ya kitamaduni, vyakula vya asili, huku mijadara na mambo mbalimbali yatakuwapo ikiwemo kufahamiana kwa pamoja kwa watu wote

whatsapp-image-2016-10-21-at-18-45-28

14680777_1297787816922145_3273963558342251532_n

Share:

Leave a reply