Auza figo mil. 60 ili kupata pesa za kuendesha maisha

510
0
Share:

Mwanaume mmoja mkazi wa Tanga anayefahamika kwa jina la Abdallah Ally ametangaza kuwa anauza figo zake ili apate pesa za kuendesha maisha.

Ally ametangaza azma yake wakati akifanya mahojiano na kituo cha runinga cha Azam Tv na kuwa ameamua kufanya maamuzi hayo kutokana na hali ngumu ya maisha.

Amesema kuwa pesa ambayo ataipata iwapo ataziuza ataitumia kuendeshea maisha yake mwenyewe na kuwasaidia ndugu zake ambao nao wana hali ngumu kimaisha.

Aidha amesema amefikia uamuzi huo baada ya kusikia baadhi ya watu wakisema kuwa figo zinahitajika sana na huuzwa kwa pesa nyingi hivyo na yeye akashawishika kuchukua uamuzi huo.

Share:

Leave a reply