Balozi Seif Ali Idd azindua mtandao wa 4G wa Zantel kwa upande wa Zanzibar

233
0
Share:

-Yawa kampuni ya kwanza kuzindua huduma ya mtandao wenye kasi zaidi Zanzibar

-Zantel pia kuongeza mara mbili upatikanaji wa mtandao Tanzania bara kufikia asilimia 80% ya watanzania.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd amezindua huduma  mpya ya mtandao wa 4G ya Zantel katika sherehe fupi iliyofanyika katika viwanja vya Kisonge mjini Zanzibar.

Zantel, kampuni ya simu inayoongoza Zanzibar, imezindua huduma hiyo mpya ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuhakikisha upatikanaji wa mtandao wa kasi na pia  kurahisisha ukuaji wa teknolojia visiwani Zanzibar.

Akizindua huduma hiyo, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd aliipongeza Zantel kwa juhudi zao za kuboresha mawasiliano ya simu visiwani Zanzibar na hasa kwa huduma hii mpya ya 4G akisema itasaidia kuimarisha maisha ya wazanzibari pamoja na kukuza uchumi.

‘Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Zantel tunajivunia sana mafanikio ya kampuni hii, na uzinduzi huu leo unatuonyesha kuwa kampuni yetu inakua na inazidi kuwanufaisha watanzania wote kiujumla’ alisema Mheshimiwa Balozi Idd.

Balozi Seif Ali Idd

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Matumizi ya teknolojia hii ya 4G yatasaidia watumiaji kupata huduma zenye ubora na uhakika na pia kuwepo kwa  ongezeko la kasi la  matumizi ya mtandao kama vile huduma ya Skype, YouTube na mitandao mingine ya kijamii.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ya mtandao wa  4G,  Afsa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu ya Zantel , Bw Benoit Janin alisema Zantel imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora na kwa urahisi zaidi .

‘Kampuni ya simu ya Zantel mara zote imekuwa ya kwanza kuleta ubunifu mpya kwa wananchi wa Zanzibar, na kwa uzinduzi wa huduma hii ya 4G Zantel inadhihirisha dhamira yake ya kuendelea  kutoa huduma bora na za kipekee kwa wakazi wa Zanzibar’ alisema Janin.

Balozi Ali Karume

Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mheshimiwa Balozi Ali Karume akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Bw.Benoit pia alisema kampuni ya Zantel itaendelea kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma za kipekee, bora na za uhakika kwa kuendelea kuwa msitari wa mbele kuzindua huduma za kibunifu zaidi.

Sambamba na uzinduzi wa huduma ya  4G, Bw.Janin pia alisema kampuni ya Zantel imefanikiwa kupanua wigo wa mtandao wake kwa upande wa bara na sasa wateja wa Zantel walioko visiwani hawana hofu wakisafiri kwenda mikoa ya bara.

‘Tumefanya upanuzi mkubwa wa mtandao wa Zantel kwa upande wa bara na tutaendelea zaidi kutanua huduma zetu lakini pia kuziboresha ili wateja wetu waweze kuzifurahia zaidi’ alisema Janin.

Toka kampuni ya Millicom inunue asilimia 85 ya hisa za kampuni ya Zantel kutoka kwa kampuni ya Etisalat, Zantel imejikita katika safari mpya kabisa ya uwekezaji mkubwa katika kupanua na kuboresha mtandao na kuboresha huduma kwa wateja wake pamoja na kuhakikisha inawapa wazanzibari na wateja wengine kiujumla huduma bora na za kisasa.

Zantel 4G Zanzibar

Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akizungumza wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Beoit Janin

Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akionyesha namna mtandao wa 4G unavyofanya kazi kwa kuzungumza kuipitia huduma ya Skype wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Zantel 4G Zanzibar

. Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi iliyounganishwa na mtandao wa 4G Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar

Benoit Janin

Ali Karume

Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi iliyounganishwa na mtandao wa 4G Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Mheshimiwa Balozi Ali Karume. Anayetazama katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd.

Benoit Janin

Waziri wa Afya, Mheshimiwa Mohamoud Thabit Kombo (kulia) akiwaeleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Benoit Janin (katikati) na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idd (kushoto) wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G wa Zantel uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Zantel 4GLTE, Zanzibar

Mfanyakazi wa Zantel akiwaunganisha baadhi ya wateja katika mtandao wa 4G wakati wa uzinduzi wa mtandao wa 4G uliofanyika katika viwanja vya Kisonge hapa mjini Zanzibar.

Share:

Leave a reply