Balozi wa Ugiriki nchini Brazil ahisiwa kuuwa mjini Rio

419
0
Share:

Polisi nchini Brazili wanachunguza kugundulika kwa mwili chini ya gari mjini Rio de Janeiro unaweza kuwa ni balozi wa Ugiriki ambaye alipotea siku tatu zilizopita

Afisa wa Polisi ambaye hakujulikana mara moja alishindwa kupatikana kwa maelezo zaidi juu ya tukio hilo la kushangaza alipotafutwa na Televisheni ya Globo

Balozi Kyriakos Amiridis 59 (pichani), alionekana mara ya mwisho siku ya Jumatatu jioni akitoka kwenye nyumba ya mke wa rafiki yake mbrazili sehemu ya Metropolitan, Polisi walisema hayo siku ya Alhamisi.

Taarifa zaidi zinasema kwamba mke wa balozi huyo aliliripoti siku Jumatano kupotea kwa mumewe wake.

Afisa wa ubalozi wa Ugiriki, amesema hawezi kuthibitisha kupotea kwa bosi wake, ila amesema kwamba yupo mapumziko huko Rio anatarajiwa kurudi Jnauari 9.

Televisheni ya Globo walionyesha kwenye taarifa yake ya habari gari nyeupe iliyounguzwa sehemu ya jirani Nova Iguacu sehemu ambayo balozi alipotea.

Balozi huyo wa Ugiriki nchini Brazili amefanya kazi kwa mara ya kwanza mjini Rio mwaka 2001 mpaka 2004 na aliwahi kuwa balozi wa nchini yake nchini Libya.

Share:

Leave a reply