Bei ya hisa za Acacia ‘DSE’ yapanda kwa 9% kutoka 5,780 hadi 6,290

294
0
Share:

Bei ya Hisa za Kampuni ya Madini ya Acacia Mining imeendelea kupanda katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo ilipanda kutoka asilimia 1.23 wiki iliyoishia Ijumaa ya Oktoba 13, 2017 hadi 9% katika kipindi cha wiki iliyoishia Ijumaa ya Oktoba 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya DSE inayotolewa kila wiki inaonyesha bei ya hisa ya Acacia imepanda kutoka Sh. 5,780 kwa hisa na kufikia 6,290.

Wakati akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko Mwandamizi DSE, Marry Kinabo alisema kupanda kwa bei ya hisa za Acacia na kampuni ya Uchumi Supermakert Ltd (14%) na KA (10%) kumepelekea ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko hilo kupanda kwa Sh. Bilioni 463 kutoka Trilioni 20.4 wiki iliyopita hadi Trilioni 20.9 wiki iliyoishia tarehe 20 Oktoba 2017.

“Ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Sh. Bilioni 205 kutoka Trilioni 9.96 hadi kafika Trilioni 10.2 wiki hii. Hii ni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za TCC (7%), TBL (3%) na DSE (2%),” alisema.

Katika hatua nyingine, Kinabo alisema Mauzo ya hati fungani katika wiki iliyoishia tarehe 20 Oktoba 2017 yamepanda hadi kufikia Bilioni 13 kutoka Bilioni 9 wiki iliyopita ya 13 Oktoba 2017
Kutokana na mauzo ya hatifungani ishirini na moja (21) za serikali na mashirika binafsi zenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 23 kwa jumla ya gharama ya Shilingi Bilioni 13.

“Thamani ya mauzo ya hisa imepungua kutoka Shilingi Billioni 30 ya wiki iliyoishia 13 Oktoba 2017 hadi Shilingi Bilioni 23 kwa wiki iliyoishia 20 Oktoba 2017.Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda kutoka hisa Mil 2.5 ya wiki iliyoishia 13 Oktoba 2017 hadi hisa Mil 2.8 ya wiki iliyoishia 23 Oktoba 2017,” alisema.

Kwa upande wa viashiria, Kinabo alisema Kiashiria cha kampuni zote zilizoorodheshwa katika soko (DSEI) kimepanda kwa pointi 48 kutoka pointi 2,124 hadi 2,172, kutokana na kupanda kwa bei za hisa za Uchumi Supermarket Ltd (USL) kampuni Kenya Airways (KA) na Acacia (ACA).Pia kishiria cha kampuni za ndani (TSI) kimepanda kwa pointi 79 kutoka pointi 3,825 hadi pointi 3,9040.

“Kiashiria cha sekta ya viwanda (IA) kimepanda kwa pointi 193 kutoka pointi 5,187 hadi pointi 5,380. Kiashiria huduma za kibenki na kifedha (BI) kimeshuka kwa pointi 16 kutpka pointi 2514 hadi pointi 2498.Kiashiria cha Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii imebaki kama awali kwenye wastani wa pointi 5,034,” alisema.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply