Benki ya Exim yatoa msaada wa vitanda na magodoro kwa hospitali ya mkoa wa Mbeya

131
0
Share:

Benki ya Exim Tanzania imetoa msaada wa vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya, wodi ya wazazi Meta, ikiwa ni sehemu ya sherehe ya miaka 20 ya kutoa huduma iliyoanza kuadhimishwa mwezi Agosti mwaka jana.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo, Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim, Bwana Stanley Kafu alisema, “ Benki ya Exim imekuwa ikisheherekea miaka 20 ya uanzilishi toka Agosti mwaka jana 2017. Kama ishara ya kushukuru  watumishi wake na jamii kwa ujumla, benki imeanzisha mpango wa kutoa vitanda na magodoro kwa hospitali nchini kote kila mwezi. Benki itaendelea mpango huu kwa mwaka mmoja hadi Julai 2018. “

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya rufaa ya Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji alipongeza benki ya Exim kwa ahadi yake ya kukabiliana na upungufu wa vitanda kwenye ma hospitali ambao unakabiliwa na taifa na kuleta juhudi zake kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya.

“Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii san a sana kwenye wodi ya wazazi.” alisema Dkt. Mbwanji.

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya imekuwa ni hospitali ya sita kupokea mchango huu, baada ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, Arusha mwezi uliopita, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya Rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana.

 

Share:

Leave a reply