Benki ya Exim yazidi kuwasogezea huduma wananchi, yafungua tawi jipya Dodoma

292
0
Share:

Benki ya Exim Tanzania imethibitisha kujitolea kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha nchini kwa kuzindua tawi jipya katika mkoa wa Dodoma, Tanzania. Utanuzi huu utaongeza uwepo wa Benki ya Exim kuwa na jumla ya matawi 33 nchini kote.

Akizungumza katika uzinduzi rasmi Fredrick Kanga, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali Watu katika Benki ya Exim Tanzania, alisema, “Utanuzi wa benki ni sehemu ya mkakati wetu wa kukuza huduma zetu katika maeneo ambayo yanatuleta karibu na wateja wetu. Tawi litatoa huduma kamili za kibenki kama vile kuhifadhi pesa, huduma za uwekezaji, na suluhisho za malipo ya kampuni.”

Tawi la Dodoma, lililopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, litawahudumia wateja wa Chuo Kikuu hiko, ambacho kina wanafunzi zaidi ya 25,000, wafanyakazi 2000 na Wizara za Serikali zaidi ya 8 ambazo zimehamia huko. Tawi litawatumikia wateja wa Jiji la Dodoma pia, kwa kuwa tawi lina umbali wa dakika 5 hadi 7 kwa mwendo wa gari kutoka katikati ya jiji.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mheshimiwa Jordan Rugimbana alipongeza Benki ya Exim Tanzania kwa kujitolea kwake, “Tunafurahi kuwa na uwepo wa Benki ya Exim katika mji mkuu wa Tanzania, ili kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi kwenye mfumo rasmi wa kifedha unaowawezesha kupata huduma, bidhaa za kifedha, na mitaji kwa jamii na watu binafsi wa Dodoma.”

Benki ya Exim ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka huu na taasisi ya The Banker ya Afrika Mashariki na sasa inasherehekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika.

 

Share:

Leave a reply