Benki ya NMB yatoa msaada kwa shule na hospitali mkoani Kagera

358
0
Share:

Benki ya NMB Tanzania imetoa msaada wa madawati kwa shule za msingi tatu na shule ya sekondari moja zote za mkoani Kagera.

Msaada huo wa madawati umetolewa kwa Shule ya Msingi Rukuraijo, Shule ya Msingi Chanyangabwa, Shule ya Msingi Rwesinga na shule ya Sekondari Isingiro.

Pia benki ya NMB imetoa msaada wa vitanda nane kwa hopsitali ya Nkwenda, vitanda vitano vikiwa vya wagonjwa na vitanda vitatu vya kujifungulia akina mama.

Gharama za msaada wa madawati kwa shule nne na kwa hospitali ya Nkwenda inatajwa kufikia milioni 25.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya NMB, Ineke Bussemaker amewatambelea wajasiriamali walionufaika na mikopo inayotolewa na NMB ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja, katika manispaa ya Bukoba.

 

 

Share:

Leave a reply