Bilioni 2.5 kuanza kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro

195
0
Share:

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imetenga jumla ya shilingi Bilioni 2.5 katika bajeti ya mwaka 2016/017 ili kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro.

Hayo yamesemwa leo,Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani Jaffo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Mjini, Mhe. Azizi Abood juu ya msongamano mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa Morogoro.

“Msongamano wa wagonjwa katika wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na kukosekana kwa hospitali ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo hilo, Serikali immepanga kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Morogoro katika bajeti ya mwaka 2016/17,” alisema Mhe. Jaffo

Mhe. Jaffo aliendelea kusema kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na jengo la wagonjwa wa nje (OPD).

Aidha, aliendelea kujibu maswali ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa kusema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary) Wilaya ya Chunya.

Chumba hicho cha kuhifadhi maiti kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230 ambapo ujenzi wa jengo utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu yatagharimu shilingi milioni 160.

Kwa sasa Wilaya hiyo ina chumba maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya kuhifadhi mati mbili tu ambacho hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo huwalazimu wahitaji kufuata huduma ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa wa Mbeya.

Share:

Leave a reply