Bill Gates aimwagia Tanzania Mabilioni, achangia sekta ya Afya Dola Milioni 15

843
0
Share:

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto leo Agosti 10,2017 imezindua  rasmi mpango wa mfumo  wa matumizi  ya Kielektroniki katika sekta ya afya  uliofanyika jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi akiwa Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda Gates Foundation, Bilionea Bill Gates ambaye taasisi yake hiyo imepanga kutoa fedha kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 15.

Katika tukio hilo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu amempongeza Bilionea huyo na Taasisi yake kwani watasaidia Wizara hiyo katika mipango yake ya kuimalisha sekta ya Afya hapa nchini. Mbali na Waziri Ummy Mwalimu, pia tukio hilo lilishuhudiwa na Waziri wa TAMISEMI, Mh. Simba Chawene pamoja na viongozi wengine wa juu ikiwemo kutoka Wizara hizo za Afya na TAMISEMI.

Awali kabla ya kuzindua mpango huo, Waziri Ummy Mwalimu alibainisha kuwa, Taasisi ya Bill and Mellinda Gates imetenga fedha hizo  na zitasaidia kuboresha mifumo hiyo ya Afya hapa nchini ambapo amebainisha kuwa, utasaidia mpango wa Wizara hiyoiliyojiwekea yaani kwa 2015/20.

Waziri Ummy Mwalimu pia amesema kuwa, Bill Gates ambaye yupo nchini kwa ziara yake maalum, aliweza kupata wasaha wa kutembelea Mkoa wa Tanga katika mpango wake wa kusaidia  tiba ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ikiwemo ya Matende na Mabusha.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika tukio hilo

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akionesha mpango wa  mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya unaosimamiwa na Taasisi ya Bilionea Billgate Bill & Melinda Gates uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya unaosimamiwa na Taasisi ya Bilionea Billgate Bill & Melinda Gates uliofanyika jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakimsikiliza kwa makini tukio hilo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya.

Waziri wa TAMISEMI, Mh. Simba Chawene akizungumza katika tukio hilo

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wakati wa tukio hilo la uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simba Chawene.

Waziri wa TAMISEMI, Mh. Simbachawene  akimkabidhi zawadi Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha kitabu cha mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam pamoja na Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates katikati na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simba Chawene. 

PICHA ZOTE NA ANDREW CHALE, MO BLOG

Share:

Leave a reply