Boko haramu wadaiwa kuuwa watu 900 mwaka 2017

74
0
Share:

Uchambuzi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kupitia takwimu zilizokusanywa na ufuatiliwaji wa shirika hilo (BBC Monitoring) unaonyesha kuwa zaidi ya watu 900 wameuliwa nchini Nigeria na kundi la wapiganaji wa Boko Haram kwa mwaka 2017.

Uchambuzi huo, umebainisha kuwa kundi la Boko Haram liliendelea kutekeleza mashambulio kila mwaka licha ya Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kusisitiza kwamba kundi hilo limetimuliwa.

Unaeleza kuwa, Boko Haram lilitekeleza jumla ya mashambulio 150 mwaka jana ikiwa ni ongezeko ukilinganisha na matukio 127 yaliyotekelezwa mwaka juzi, ongezeko hilo limetokana na kauli ya Rais Buhari kudai kuwa kundi hilo limesambaratishwa.

Uchambuzi huo umeeleza mbinu zilizotumiwa na kundi hilo ikiwemo kutekeleza mashambulio 90 ya kujihami na 59 ya kujitoa muhanga katika kipindi cha mwaka 2017.

Mashambulio ya kujitoa muhanga yalitumika sana katika mji wa Maiduguri ambao ni kitovu cha uasi, huku jimbo la Borno ulikoanzia uasi huo likitajwa kuathirika sana na mashambulio hayo.

Share:

Leave a reply