Bomu laua 29 na kujeruhi 166 katika uwanja wa mpira mjini Istanbul

363
0
Share:

Watu 29 wamekufa na wengine 116 kujeruhiwa baada ya kutokea milipuko miwili ya bomu usiku wa kuamkia leo nje ya uwanja wa mpira mjini Istanbul, Uturuki.

Makamu Waziri Mkuu Numan Kurtulmus amesema mashambulio hayo yalitokana na bomu lililotegwa kwenye gari na jingine la muhanga ambapo askari wawili wamepoteza maisha huku 17 wakifanyiwa upasuaji na wengine sita wakiwa kwenye chumba cha uangalizi maalum.

“Muhanga huyo alifyatua bomu sekundi 45 baada ya bomu la kwenye gari kulipuka”, alisema Makamu Waziri Mkuu Numan Kurtulmus katika mkutano na waandishi wa habari.

Amesema hadi sasa watu 10 wanashikiliwa kutokana na tukio hilo.

turkey-explo

Askari walipowasili kwenye eneo la tukio usiku wa kuamkia leo. (Picha na Reuters/Murad Sezer)

Share:

Leave a reply