Bomu laua watu 13 Mogadishu, Al Shabab wathibitisha kuhusika

299
0
Share:

Watu wanaokadiriwa kufikia kumi na tatu wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika magari mawili yaliyokuwapo karibu na Uwanja wa Ndege wa Mogadishu, Somalia.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya tukio hilo moshi mkubwa ulionekana kutanda katika eneo ya ofisi kuu za Umoja wa Afrika (AU) ambao wapo nchini humo kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama na amani.

Inaelezwa kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea karibu la sehemu ya ukaguzi na lingine likitokea karibu na lango la kuingi katika Uwanja wa Ndege wa Mogadishu na kusababisha vifo va watu hao ambao tisa wanatajwa kuwa askari wa kulinda amani na watatu ni raia wa kawaida.

Hata hivyo tayari kikundi cha Al Shabab kimesema kinahusika na tukio hilo na kilikuwa kinalenga kufanya mlipuko huo katika makao makuu ya AU katika nchi hiyo.

Share:

Leave a reply