Bomu laua zaidi ya wakimbizi 40 wa Somalia

746
0
Share:

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia (UNHCR) limesema idadi ya wakimbizi wa Somalia ambao wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika boti walilokuwa wamepanda ni zaidi ya watu 40.

Msemaji wa UNHCR nchini Yemen, Shabia Mantoo alihibitisha kuwepo kwa idadi hiyo ya watu ambao wamepoteza maisha ijapokuwa hadi sasa bado hawajapata taarifa rasmi ni watu gani wamehusika na shambulio hilo ambao limeua watu hao.

Shabia alisema kwa sasa bado hawajaelewa nini hasa kimekuwa chanzo kwani watu hao walikuwa wakisafiri tu na tukio hilo limewapata wakati wakiwa katika pwani ya Hodeidah.

Inaelezwa kuwa wakimbizi hao wa Somalia walirushiwa bomu na helikopta katika boti waliyokuwa wamepanda wakati wakitoka nchini Yemen kuelekea Sudan.

Share:

Leave a reply