Brazil yazuia matumizi ya WhatsApp kwa masaa 72, WhatsApp wajibu

214
0
Share:

Wananchi wa Brazil watakosa huduma ya WhatsApp katika simu na vifaa vingine kwa siku tatu kufuatia kufungwa kwa matumizi ya app hiyo ikiwa ni kama adhabu kwa mmiliki wa WhatsApp.

Hatua ya kufungiwa kwa WhatsApp imetolewa na Jaji mmoja nchini humo, Marcel Montalvao kwa madai kuwa mmiliki wa WhatsApp ambaye pia ndiyo mmiliki wa Facebook ameshindwa kutoa taarifa za mtumiaji wa mtandao katika kesi iliyo mahakamani.

Kufungwa kwa huduma hiyo kulianza jana 17:00 ambapo hakutakuwa na huduma hiyo kwa masaa 72 na baada ya hapo huduma itarejea kama awali.

Baada ya kufungiwa, WhatsApp nao wamejibu kuwa wanashangazwa na jambo hilo kuwanyima wateja wao huduma yao kwa taarifa ambayo wameshaitolea majibu.

“Haya maamuzi ya kuwaadhibu zaidi ya Wabrazil milioni 100 ambao wanatumia huduma zetu kwa ajili ya kutulazimisha sisi kutoa taarifa, tunarudia tena hatuna hiyo taarifa,” ilisema taarifa hiyo.

Share:

Leave a reply