Muigizaji Lulu ahukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani

1005
0
Share:

Msanii Elizabth micheal ‘Lulu’ amehukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.

Lulu alikuwa akituhumiwa kumuua muigizaji mwenzake Steven Kanumba mwaka 2012 ambaye ilielezwa kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Wakili wa Lulu, Peter Kibatala amesema watakata rufaa kufuatia Mahakama Kuu kumhukumu mteja wake kifungo cha miaka miwili gerezani.

 

NEWS UPDATES: Wakili Peter Kibatala amewasilisha kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga hukumu ya Mahakama Kuu ya kumfunga mteja wake miaka miwili.

Share:

Leave a reply