British Council waendesha mafunzo ya lugha bure ndani ya Sabasaba

666
0
Share:

British Council Tanzania ambao wapo katika banda la Jakaya Kikwete kwenye mabanda ya Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam wametoa ofa kabambe ya Mwananchi anayefika kwenye banda lao hilo kuweza kujipima uwezo wa lugha ya kiingereza ‘English test’ ambayo itamsaidia katika kujua uwezo pamoja na fursa mbalimbali zinazotolewa na British Council.

Wakizungumza na wanahabari leo Julai 5,2017, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata ofa ya kujipima bure masomo ya lugha ya kiingereza ambayo itawasaidia katika kujua uwezo wao wa kuongea/ kuandika lugha hiyo ambayo inatumika karibu Duniani kote.

 Mkurugenzi Mkazi wa British Council Tanzania, Bi.Angela Hennelly amebainisha kuwa, wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwawezesha wananchi wake kujua lugha hiyo ya kiingereza ambayo imekuwa ikitumika Duniani kote ikiwa pia moja ya lugha ya kibiashara baadhi ya maeneo.

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania. British Council  ipo hapa Tanzania kwa sasa inakaribia miaka 47, tunasaidiana katika kusimamia mitihani mbalimbali pamoja na kutoa kozi za lugha hii ya Kiingereza ‘English Course’.

Tunawakaribisha wananchi wote wafike waweze kujipima uwezo wao wa lugha hii ambayo hapa tunafanya bure kabisa bila malipo yoyote.” Ameeleza Bi. Angela Hennelly.

British Council wanatoa mafunzo ya kozi mbalimbali katika lugha ambayo ni msaada mkubwa kwa watanzania  ambao wanapitia hapo kuweza kujifunza pindi wanapojiandaa kwenda kusoma nje ya nchi ama katika uwelewa fasaha wa lugha hiyo.

Aidha, zoezi hilo la kujipima uwezo wa lugha hiyo ‘English test’ inafanyika kila siku bila malipo kwenye banda hilo la Jakaya Kikwete ndani ya Sabasana, ambapo baada ya hapo  wataendelea na utararibu huo kwa malipo ya Tsh. 48,000, kwa wananchi watakaotaka kujifunza kwa ofisini kwao, Posta Barabara ya Samora, Jijini Dar e Salaam.

Mkurugenzi Mkazi wa British Council Tanzania, Bi.Angela Hennelly akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani wakati wa tukio hilo) mapema leo Julai 5,2017 katika maonyesho ya Sabasaba

Bi. Angela akifanya majadiliano na wananchi waliofika kwenye banda hilo

Baadhi ya wananchi wakiendelea na zoezi la ‘English test’ katika banda la British Council

Mkurugenzi Mkazi wa British Council Tanzania, Bi.Angela Hennelly akifanya majadiliano na baadhi ya vijana walifika katika zoezi hilo la kujifunza lugha ya kiingereza bure kwa kipindi hiki cha Sabasaba tukio hilo mapema leo Julai 5,2017 katika maonyesho hayo ya Sabasaba (Picha na Stori: Andrew Chale-MO BLOG).

Share:

Leave a reply