“CCM kwenda na wakati ndio siri ya ushindi”- Kinana

158
0
Share:

Baada ya Chama cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mdogo wa Udiwani uliofanyika Novemba 26, 2016 ambapo ilizoa kata 42 kati ya 43, chama hicho kimetaja siri ya kushinda kwenye uchaguzi huo pamoja na chaguzi mbalimbali zilizofanyika nchini. 

Akizungumza wakati wa akitoa taarifa ya chama katika kipindi cha miaka mitano kwenye Mkutano Mkuu wa CCM unaoendelea mjini Dodoma, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema ilani bora, uteuzi wa wagombea bora sambamba na chama hicho kwenda na wakati, ndio siri ya kushinda katika uchaguzi.

“Ilani bora, uteuzi wa wagombea bora, CCM kwenda na wakati, ndio chanzo cha ccm kushinda kwenye uchaguzi,” amesema. 

Aidha, Kinana amesema uwepo wa demokrasia ndani ya CCM ikiwemo uhuru wa wanachama kuchagua na kuchaguliwa na wa kutoa maoni, mawazo na hoja, pamoja na utaratibu mzuri wa kuchuja wagombea, ndio sababu ya chama hicho kukubalika. 

“Kinachofanya chama chetu kuwa imara ni demokrasia ndani ya chama, demokrasia ya haki ya mwanachama kuchagua na kuchaguliwa, mwanachama yeyote anaweza kugombea nafasi yoyote.jambo la pili kukubalika ni watu kuwa huru kutoa hoja na maoni ndani ya chama, wajumbe wana uhuru wa kusema,” amesema.

Kinana amesema kuwa, kwa mwenedo huo wa CCM, inatarajia kupata asilimia nyingi ya kura katika chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019, na uchaguzi mkuu 2020.

Share:

Leave a reply