CDEA yaendesha mafunzo ya IIDEA 2017 kwa wabunifu mavazi na urembo wa Afrika Mashariki

639
0
Share:

Wabunifu wa mavazi na urembo kutoka nchi za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania na Uganda, wamepigwa msasa wa namna ya kuendesha na kukuza fani zao kwenye sekta za ubunifu na biashara  IIDEA 2017,mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika lisilo la kiserikali (Culture and Development East Africa –CDEA) la jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuongeza ujuzi na elimu ya biashara pamoja na masoko ambapo mafunzo hayo yanafadhiliwa na GIZ  tawi la Afrika Mashariki.

Awali akizungumza katika mafunzo hayo ambayo  yalikuwa ya siku nne, Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Bibi Ayeta Wangusa alishukuru na kuwapongeza washiriki kwa kuchaguliwa kwenye  mradi huo ambao ni wa kwanza na wa kipekee katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ukiwa chachu katika kuinua uchumi kwa kupitia sekta ya ubunifu huku akiwataka washiriki hao kuzingatia  yale yote watakayofundishwa hususani suala la kutafuta masoko nje ya mipaka  ya nchi zao wanazotoka.

Mafunzo hayo yalihusisha jumla ya ya washiriki 17 ambao walibahatika kuchaguliwa waliweza kujengewa uwezo na mbinu mbalimbali ikiwemo zaUbunifu wa mavzi, Biashara, Mtandao, Sheria  na  mbinu tofauti za kupata ufadhili.

Aidha, miongoni mwa walimu waliotoa mafunzo hayo, wakiwemo Bibi Santa Anzo  na Bibi.Bernadine Buzabo kutoka nchini Uganda, waliweza kutoa mafunzo na mbinu za ubunifu na kufanya mauzo ya kazi zao ikiwemo kwenye masoko tofauti ya ndani na nje ikiwemo Afrika, Ulaya na Amerika.

Washiriki hao pia walipata wasaha wa kujifunza namna ya kuandaa Mpango wa kazi zao za biashara na usajiri wa biashara ikiwemo kusajiri kampuni pamoja na kujitengenezea majinna (branding).

Mafunzo hayo ya  siku nne, yaliwawezesha washiriki kupata wasaha wa kutumia bidhaa halisi za ndani ya nchi za  Afrika Mashariki ikiwemo khanga zilizotengenezwa na pamba  ya hapa nchini Tanzania, Ngozi halisi ya mbuzi, Shanga na  simbi ambazo zitokanazo na zao la baharini ambazo pia zilikuwa kivutio katika kazi zao hizo.

Kwa upande wao waratibu wa mafunzo hayo, wamebainisha kuwa,wamedhamilia kutumia bidhaa za asili ili kukuza uchumi katika  ngazi zote za mnyororo wa thamani katika sekta ya ubunifu wa mavazi na mitindo.

Mradi huo pia unajulikana kama Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA)  unaratibiwa na CDEA kwa ufadhili wa GIZ East Africa, ukiwa na lengo la  kukuza ujuzi na elimu ya biashara kwa sekta ya filamu, muziki na ubunifu wa mavazi huku kwa sasa ukihusisha nchi mbili za Afrika Mashariki  ikiwemo Tanzania na Uganda.

Kwa sasa mafunzo hayo ya Atamishi ya kazi za Sanaa (IIDEA) yameanza na masuala ya ubunifu wa mavazi na urembo ambapo pia yatafuatiwa na mafunzo mengine ikiwemo Muziki na filamu.

Tazama hapa matukio mbalimbali ya picha ya mafunzo hayo:

Washiriki ambao ni wabunifu kutoka Afrika Mashariki akiwemo Andrew Kalema, Joyce Gerald (katikati) na Makeke Jocktan wakifuatilia mafunzo hayo

Washiriki na wataalamu wakibadilisha mawazo wakati wa semina magunzo hayo

Bi Amal Mohamed  kutoka Kenya akitoa mafunzo ya namna ya kupata Ufadhili kupitia ubunifu kwa wabunifu wa Afrika Mashariki

Bi Bernadine Buzabo akiwasilisha mafunzo kwa washiriki kwa njia ya mtandao wa Skype kwa washiriki (Hawapo pichani)

Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa akitoa takwimu za fashionomics kwa washiriki wa mafunzo hayo

Mmoja wa wanufaika wa ufadhili kupitia ubunifu kutoka Kenya Bwana James Otieno  akitoa mafunzo kwa washiriki

Baadhi ya washiriki Ester Kiula na Whitnery Gnaj wakifuatilia mafunzo hayo

Mshiriki kutoka Uganda, John Okello akishona vazi alilobuni mwenyewe wakati wa mafunzo hayo

Kemi Kalikawe kutoka Tanzania akipitia mchoro wa mshiriki Clare Musila (Uganda) wakati wa mafunzo hayo

Mshiriki akimuonesha mkufunzi kazi yake namna ya inavyovaliwa

Mshiriki akipata maelekezo ya vipimo toka kwa mkufunzi

Kemi Kalikawe akimuelekeza Catherine Mood Board

Mshiriki Victoria Joseph akiwa kwenye ubunifu wake

Kebirugi Nina akishona vazi alilobuni

Whitney Gnaj akijaribu vazi alilolibuni

Kemi Kalikawe  akipitia mchoro wa Clare Musila 

Wakili masuala ya miradi na biashara Bi. Sia  Mrema akifundisha kuhusu usajili wa biashara na makampuni kwa washiriki hao ili kujitangaza zaidi hasa kupitia majina yao ya ubunifu (brand).

Bibi Santa Anzo ambaye ni mbunifu mkongwe na mahiri nchini Uganda akitoa mafunzo ya namna ya wabunifu watakavyoweza kubuni ubunifu wao na kuuza bidhaa zao  katika masoko ya nje.

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akipitia kazi ya mwanafunzi Clare Musila

Aliyewahi kuwa Miss Tanzania kipindi cha nyuma, Bi. Nasreen Karim akitoa mafunzo kwa wabunifu hao (Hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya IIDEA 2017.

Mmoja wa walimu wakitoa mafunzo katika mafunzo hayo.

Vazi la mbunifu wa Tanzania Makeke Jocktan alilolibuni wakati wa mafunzo hayo.

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Wabunifu wakiendelea na ubunifu wao

Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Baadhi ya vitu vilivyotengenezwa na wabunifu hao katika mafunzo ya IIDEA 2017

Kazi za wabunifu zilizofanywa na washiriki

Baadhi ya washiriki wabunifu na walimu wakipiga picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa CDEA, Bibi Ayeta Anne Wangusa.

Picha ya pamoja ya washiriki wote wakipiga baada ya kumaliza mafunzo hayo ya IIDEA 2017.

Share:

Leave a reply