CDEA yaendesha mafunzo ya utayarishaji filamu

636
0
Share:

Waandaaji filamu chipukizi ishirini na mmoja (21) wameshiriki katika mafunzo ya siku mbili yaliyoandaliwa na atamishi ya kazi za sanaa ya shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Afrika (CDEA) siku ya ijumaa na jumamosi tarehe 20-21 2017. Mafunzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Eco sanaa Uliopo Mikocheni B jijini Dar es salaam.

Wasanii Hawa waliitikia wito uliotolewa kwenye kurasa za kijamii za shirika la CDEA ambapo ilittamka kuwa wajisajili kama wana nia ya kujifunza jinsi ya kuboresha filamu zao na kupanua maoko hususani soko la mtandaoni.  “Hii ni fursa ya kujifunza Zaidi mbinu za kujupatia fedha kwa uuzaji wa filamu” Bi Angela Kilusungu ambaye ni afisa mradi akielezea juu ya wito huo.

Mafunzo haya yapo chini ya mradi mkubwa wa Incubation for Integration and Development in East Africa(IIDEA) yanayofadhiliwa na GIZ EAC kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa leongo la kukuza mshikamano wa nchi wanachama wa jumuiya kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo sanaa ambapo  atamishi ya kazi za sanaa ya CDEA inaingia.

Chini ya mradi hii wa IIDEA CDEA inakutaisha nchi mbili za wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashriki ambazo ni Tanzania na Uganda. Ambapo Muendesha mafunzo Bw. Matthew Chan-Piu ametokea Uganda na amekutana na watanzania ili kubadilishana nao ujuzi wa utengenzaji filamu bora kwa ajili ya masoko.

“Tungependa kuona filamu zinazozalishwa kwa ushirikiano baina ya watu wa nchi hizi mbili, faida yake ni kupanua soko za filamu hizo na mwishowe kukuza kipato cha watayarishaji wa filamu hizo.” Amesema Bi Kilusungu akifafanua zaidi lengo la mafunzo hayo.

Kwa kuona hilo CDEA imemleta Nchini Bwana Matthew Chan-Piu aliye chini ya Maisha Film Labu ya Uganda ili kuwafa a vijana wetu chipikizi kufikiwa malengo ya kuwa na ushindani katika soko la filamu la Afrika mashariki na la dunia kupitia mfumo wa kuuza kwenye mtandao.“Bwana Chan-Piu Anafanya vizuri sokoni hivyo tumeona aje awafunze watanzania juu ya fursa hiyo”  Ameendelea Bi Kilusungu.

Kwa upande wake Bwana Chan-Piu amewaeleza watayarishji chipukizi kuwa yeye anaamini msingi wa upatikanji wa soko la filamu unaanzia kwenye hatua ya kwanza ya utayarishaji ambayo ni utengenezaji wa muswada wa filamu kwa lugha ya kigeni Scripts. Akaenelea kwa kuwaonesha jinsi yeye anvyyo andika miswada yake na anavyopanga ratiba yak echini ya muswada husika mpaka masoko filamu inapokua tayari.

Bwana Chan-Piu amewaonesha watayarshashi programu iitwayo Celtx ambayo inatumika kunadalia miswada na amewafundisha jinsi ya kuitumia. Mwisho wa mafunzo hayo ya siku mbili wasanii washiriki wanatakiwa kumtumia kazi fupi ya kurasa mbili ambayo wameandika kutumia technolojia hiyo ili waweze kujujengea uzoefu wa kuitumi katika kazi zao za kila siku.

Ili wazasnii waweze kuzowea kuuza bidhaa zao mtandaoni CDEA imeandaa tovuti iitwayo SanaaBiz Portal. Ambapo wasanii wa fani mbalimbali zikiweo filamu, muziki, fasihi na ubunifu mitindo wanweza kuweka bodhaa zao na kuuza kwenye soko la mtandaoni ambalo linalokuwa kwa kasi.

Mafunzo haya ya filamu  nduyo yanayofunga mradi wa atamishi za kazi za sanaa waCDEA. Mradi hii ulikuwepo kwa muda wa mwaka Mmoja na ulizindulilwa mwezi Noveba Mwaka jana. Mpaka sasa wasanii 89 wa fani za filamu, Muziki, na ubunifu mavazi na mitindo wameweza kunufaika na mafinzo yaliyo andaliwa ili kuwaongezea ujui wa kitaluma na Kibiashara wa kiskata .

 

Share:

Leave a reply