Chama cha ADC chawakingia kifua wafanyabiashara wa mafuta

418
0
Share:

Chama Cha Alliance for Democratic Change (ADC) imeitaka Mamlaka ya Mapato nchini TRA kusitisha zoezi la kuvifungia vituo vya mafuta nchini kwa kuwa limewakosesha huduma watanzania wengi ambao kimsingi hawana hatia na hadha wanayoipata.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu ADC, Doyo Hassan Doyo, alisema kuwa ni vyema serikali ikawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa vituo hivyo vya mafuta na kuruhusu huduma ziendelee kwani huduma ya mafuta imeendelea kuwa tatizo kwa wananchi wa maeneo mbalimbali nchini.

“Mamlaka ya Mapato nchini ipo katika oparesheni ya kuvifungia vituo vya mafuta nchini ambazo havijafunga mashine za EFD katika ‘Pump ‘ za mafuta jambo ambalo halichochei ukusanywaji wa mapato wenye ukweli wa takwimu,” alisema.

Katika hatua nyingine, Doyo alisema ADC inakitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kutoingilia Mgogoro ulikuwepo Ndani ya Chama cha Wananchi CUF.Ambapo amesema kuwa Chadema kuingilia Mgororo wa CUF kunaweza kuhatarisha amani ya nchi. 

Hata hivyo Doyo ameitaka serikali iviache vyama vya siasa nchini vifanye shughuli zao.

ADC ipo katika maandalizi ya Maadhimisho ya kuzaliwa kwa Chama hicho ambayo yatafanyika Tarehe 22 Agosti Mwaka Huu ambapo chama hicho kitakuwa na ziara kwenye asasi za Kiraia, kuwatembea Wagonjwa, Wafungwa, Vyuo vikuu na Kutembea Nyerere Foundation ,N.K  na Mwisho kuhitimisha kwenye Ofisi za chama hicho Buguruni Jijini Dar es Salaam, huku vyama mbalimbali vikialikwa.

Na Regina Mkonde 

Share:

Leave a reply