CMSA yazindua shindano kwa wanavyuo

278
0
Share:

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) jana Jumatatu, Julai 4, 2016 imezindua shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu Juu ya Tanzania kwa mwaka 2016.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bibi Nasama M. Massinda alisema shindano hilo lina lengo la kuongeza ueledi na ufahamu kuhusu masoko ya mitaji kwa wanavyuo hapa nchini hali ambayo inatarajia kuchangia ongezeko la ushiriki wa Watanzania kama wawekezaji, watoa dhamana na wataalum wa kutoa huduma katika masoko ya mitaji pindi wanapohitimu masomo yao.

‘Shindano hili lijulikano kama Capital Markets University Challenge lina sehemu mbili – insha na sehemu ya maswali kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo na taasisi za elimu ya juu, alisema Bi Massinda huku akiongeza kuwa wanafunzi watapata fursa ya kuongeza elimu juu ya kuwekeza akiba kwa njia endelevu na kuongeza matumizi ya Tehama kwa wanavyuo.

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Massinda

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nasama Massinda akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Julai 4, 2016. 

Wanavyuo watashiriki Shindano la maswali na majibu kwa kutumia simu za kiganjani kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwenda namba 0766 046046, na kwa kutumia tovuti na mtandao wa kompyuta. Kwa upande wa insha, wavyuo wanatikiwa kuandika insha kuhusu fursa na faida za kutumia masoko ya mitaji katika miradi ya maendeleo nchini. Insha hiyo inatakiwa isizidi kurasa nne (4) na kutuma kwa barua pepe kwenda challenge@cmsa-tz.org. Mshindi wa jumla katika kila shindano atapata zawadi ya 1,800,000/- huku mshindi wa pili akipata 1,400,000/-. Pia washindi kutoka vyuo vitatu bora – wavulana na wasichana, watapata fursa ya safari ya wiki moja kutembelea makao ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana jijini Dar es Salaam.

Capital Markets University Challenge ilizinduliwa mwaka jana ambapo liliendeshwa kwa mafanikio makubwa na kuvuka lengo la ushiriki kwa zaidi ya 300%. ‘Mafanikio hayo yalitokana na jitihada za kuhamasisha matumizi ya technolojia ya habari kwa matumizi ya simu za kiganjani, mtandao wa kompyuta, barua pepe na wavuti, asema Bi Massinda huko akiongeza kuwa mafanikio hayo yaliandika historia mpya katika sekta ya masoko ya mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

Shindano ya Capital Markets University Challenges ilizinduliwa tarehe 4 Julai 2016 na likafika tamata Agosti 15, 2016.

Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipangowa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama
Mkurugenzi wa Utafiti, Sera na Mipangowa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Shindano la insha na maswali kuhusu Masoko ya Mitaji kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam Julai 4, 2016.
Share:

Leave a reply