DAS Ilala:”Wazazi DSM wanaongoza kwa kutelekeza watoto wenye ulemavu”

639
0
Share:

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu katika mkoa wa Dar es Salaam wanadaiwa kuongoza kwa kutelekeza watoto wao katika shule maalumu za walemavu hasa zilizopo katika wilaya ya Ilala.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa Ilala, Edward Mpogolo katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu yaliyofanyika Disemba 3, 2016 katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

Mpogolo ameyasema hayo wakati akieleza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu katika mkoa wa Dar es Salaam.

“Dar ina shule za watu wenye ulemavu nne, 3 zipo Ilala. Wazazi na walezi hao wamekuwa wakiwapeleka watoto katika shule hizo kwa lengo la kupata elimu kisha kuwatelekeza,” amesema.

Ametaja changamoto nyingine zinazowakabili walemavu kuwa ni umasikini kutokana kwamba hakuna mfumo mzuri wa kuwawezesha kiuchumi na ubaguzi dhidi yao.

“Changamoto nyingine ni ubovu wa miundombinu ya shule hizo sababu ni za kizamani zilijengwa muda mrefu, serikali tunaiomba itusaidie namna ya kuziboresha shule hizo,” amesema.

Share:

Leave a reply