David Kafulila ajiunga rasmi CCM

587
0
Share:

Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini (2010-2015), David Kafulila amejiunga na chama cha Mapinduzi (CCM).

Kafulila amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole katika mkutano wa kampeni za udiwani Mbweni jijini Dar es Salaam.

Kada huyo kabla ya kujiunga na CCM alikuwa ni mwanachama wa Chadema ambapo alitangaza kujivua uancahama wa Chadema siku ya jumatano Novemba 22, 2017.

Kafulila alisema sababu ya kujivua uanachama wa Chadema ni kutokuwa na imani kwa vyama vya upinzani katika vita ya ufisadi.

“Kwa kuwa sina tena imani na upinzani kama jukwaa salama la kupambana na ufisadi, nimeamua kwa hiari na utashi wangu kujivua uanachama wa CHADEMA,” ilieleza sehemu ya barua ya Kafulila kujivua uanachama wa Chadema.

Share:

Leave a reply