DC Hapi ampa siku saba Mkurugenzi kuondoa magari yaliyoegeshwa maeneo yasiyo rasmi

702
0
Share:

Kufuatia changamoto ya baadhi ya magari na malori kuegeshwa kwa muda mrefu kinyume cha sheria, katika barabara za mitaa na kusababisha uharibu wa miundombinu hasa mitaro pamoja na kusababisha msongamano wa magari.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Happy amemuagiza Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Aaron Kagulumjuli  kuyaondoa magari na malori yaliyoegeshwa katika sehemu zisizo rasmi ndani ya siku saba kuanzia leo, ikiwa ni pamoja na yadi bubu za uuzaji wa magari.

Hapi ametoa maagizo hayo Februari 21, 2017 katika ziara yake kwenye kata ya Mzimuni iliyoko wilayani Kinondoni ambapo ametembelea miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa maji katika mtaa wa Mtambani, ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Mzimuni, na soko la magomeni .

“Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni  nakuagiza magari na malori yote yaliyoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi yatolewe, tafuta breakdown yakaondolewe. Yatakapo ondolewa mmiliki atalipa faini ya kosa pamoja na gharama za kila siku gari itakapo kaa,” amesema.

Share:

Leave a reply