DEAL DONE: Manchester United yakamilisha uhamisho wa Paul Pogba

201
0
Share:

Ile ndoto ya mashabiki wa Manchester United kumuona mchezaji wao wa zamani, Paul Pogba akijiunga tena katika klabu hiyo imetimia baada ya Man United kukamilisha usajili wa kiungo huyo.

Pogba amerejea Man United akitokea Juventus alipokuwepo tangu mwaka 2012 na amerudi katika klabu yake ya zamani kwa kitita cha Pauni Milioni 89 kwa mkataba wa miaka mitano.

Akizungumza na mtandao wa Manchester United baada ya kukamilisha uhamisho huo, Pogba alisema ni furaha kwake kurejea katika klabu iliyomkuza katika soka na amewasili klabuni na kukuta watu ambao aliwahi kuwa nao katika timu moja ya vijana na sasa anajipanga kufanya kazi na kocha Mourinho.

“Nina furaha kurejea United, ni sehemu maalum kwa moyo wangu na sasa naangalia mbele zaidi kufanya kazi na Jose Mourinho,

“Nilikuwa na furaha wa kipindi nilichokuwa Juventus na kuwa na wakati mzuri wa kuweka kumbukumbu kwa klabu na wachezaji ambao nawahesabu kama marafiki,” alisema na kuongeza.

“Lakini nilihisi ulikuwa ni muda sahihi kurejea nyumbani Old Trafford na nitakuwa na furaha kama nikicheza mbele ya mashabiki wa Man United natamani muda ufike nianze majukumu yangu katika timu, hapa ni sehemu sahihi ambayo ninaweza kufikia kila jambo ambalo ninataka kulifanya katika ngazi ya klabu”

Share:

Leave a reply