Dele Alli atengewa Pauni 800,000 kwa wiki na klabu za China

735
0
Share:

Baada ya Oscar, Carlos Tevez na John Mikel Obi kujiunga katika klabu za China, timu hizo zinaonyesha nia ya kuendelea kuimarisha ligi kuu ya nchi hiyo kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa ili kuifanya ligi yao kuwa maarufu kama zilivyo ligi nyingi za Ulaya.

Kwa sasa klabu hizo zinaonekana kugeuzia majeshi kwa kiungo wa Tottenham, Dele Alli ambye kwa siku za karibuni anaonekana kiwango chake kuzidi kuwa bora hivyo klabu za China zikiamini kuwa atasaidia kukuza ligi ya nchi hiyo.

Dele Alli anatajwa kuwa atakuwa akipokea Pauni 800,000 kwa wiki, mshahara ambao kwa namna moja au nyingine unaweza kuchangia kumshawishi kuwa tayari kuondoka Uingereza na kwenda kucheza China.

Licha ya Dele Alli pia wapo wachezaji wengie ambao wanatajwa kuhitajika na klabu za China kuwa ni pamoja na Harry Kane, Ross Barkley, Daniel Sturridge, Harry Kane, John Terry na Wayne Rooney.

Share:

Leave a reply