Dereva aliyesababisha ajali iliyoua wanafunzi 2 Gongo la Mboto akamatwa

570
0
Share:

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, limesema ajali iliyotokea mapema leo maeneo ya Superdoll barabara ya Nyerere ambapo lori aina ya Scania na gari aina ya Eicha ziligongana uso kwa uso, imesababisha vifo vya wanafunzi wawili na majeruhi 24.

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari Mei 3,2017 ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori linalomilikiwa na kampuni ya Mikoani Traders, ambapo aliingia barabara ya pili pasipo kuchukua tahadhari kwa nia ya kuingia kwenye maegesho ya ofisi yao na kusababisha ajali hiyo.

“Lori aina ya scania lenye namba za usajiri T.273 CEV liligongana uso kwa uso na gari aina ya Eicha T.376 DFT lililokuwa likitokea gongo la mboto. Dereva wa lori hilo amekamtwa kwa mahojiano zaidi na magari hayo yako katika kituo cha polisi cha Chang’ombe,” amesema.

Ametaja majina ya wanafunzi waliofariki dunia kuwa ni Itlam Wema Athumani mwanafunzi kidato cha kwanza shule ya sekondari Msimbazi na Sakina Hamis Imamu mwanafunzi kidato cha kwanza shule ya Sekondari Mchikichini.

Aidha, amesema majeruhi walipelekwa hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu na kwamba 21 wameruhusiwa, huku watatu wakiendelea na matibabu hospitalini hapo.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply