Dereva bodaboda auawa kwa kuchomwa kisu shingoni

242
0
Share:

Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la William Nasson  (22) ambaye ni dereva bodaboda anaepaki kituo cha ujenzi na mkazi wa Kilimahewa Manispaa ya Kigoma Ujiji amefariki dunia baada ya kuchomwa kitu chenye ncha kali shingoni na watu wasiojulikana.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Kigoma ACP Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Octoba 15 majira ya saa 4 usiku huku akisema kuwa hadi sasa eneo ambalo marehemu alichomwa kisu halijafahamika.

“Marehemu alianguka ghafra maeneo ya kituo cha daradara Maweni akiwa na pikipiki yake yenye namba za usajiri MC569BSE aina ya King Lion akitokea burega wakati akielekea hospital ya rufaa Maweni kwa lengo la kupatiwa matibabu” amesema Kamanda Otieno.

Aidha kufuatia kifo hicho kamanda Otieno ametoa wito kwa madereva wa pikipiki mkoani Kigoma kuwa makini hasa nyakati za usiku kwa kukodiwa na watu wasiowafahamu kutokana na watu wenye nia mbaya kutumia mwanya huo kuwateka na kuwaua.

Hata hivyo mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma Maweni na kubaini kuwa marehemu amefariki baada ya kupoteza damu nyingi kutokana na jeraha alilopata baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali  na tayari mwili huo umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Na Emmanuel Michael, Kigoma 

Share:

Leave a reply