Diamond Platnumz, Nandy mikononi mwa Polisi

178
0
Share:

Waziri wa Habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amelieleza Bunge kuwa mwanamuziki Naseeb Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz jana alikamatwa na kuhojiwa na Polisi kwa kusambaza picha zilizokosa maadili katika mitandao ya kijamii.

Dkt. Mwakyembe amesema mwanamuziki Nandy na yeye amehojiwa na kama watapatikana na makosa watapelekwa mahakani ili hatua zichukuliwe dhidi yao.

“Kuna baadhi ya wasanii wetu walianza kufanya uhuni uhuni kwenye mitandao ya kijamii, jana tumeweza kumkamata mwanamuziki nyota Tanzania Diamond tumemfikisha Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha vilevile imebidi hata binti Nandy imebidi apelekwe Polisi kwa kuhojiwa. Tunaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani,” amesema Waziri Mwakyembe na kuongeza.

“Naomba nitoe wito kwa vijana wote nchini, mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu zotw ambao umezuiwa na sheria zingine hii nchi ina utamaduni wake, tunahitaji kulinda, kizazi cha leo, cha kesho na kesho kutwa cha Taifa hili.”

Share:

Leave a reply