DIWANI WA CCM AJIUZULU KAMATI YA FEDHA,KUPISHA TUHUMA ZA UBADHIRIFU SHINYANGA

325
0
Share:

Aliyekuwa Naibu mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga na sasa Diwani wa Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga, David Mathew Nkulila (CCM) ametangaza kujiuzulu ujumbe wa Kamati ya Fedha na Utawala ili kufikisha ujumbe kwa umma kwamba hakubaliani vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma unaofanyika katika Manispaa ya Shinyanga.

Miongoni mwa hoja zilizomfanya ajiuzulu ni sakata la Greda aina TEREX T180 mali ya Halmashauri Manispaa ya Shinyanga,hoja za barabara za lami mjini Shinyanga,hoja kuhusu JASCO, udanganyifu wa Bajeti 2016/17 ulioanzishwa na Baraza la madiwani na uliowasilishwa wizarani sambamba na ujenzi wa nyumba za ghorofa mjini kati na usimamizi wake.

Mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambaye pia mstahiki meya wa manispaa hiyo Gulam Hafeez Mukadam amesema  hapingani na taarifa za wataalam waliochunguza kuwa greda lililonunuliwa na manispaa hiyo kuwa ni zima na halina tatizo.

Hata hivyo amesema bado hajapata taarifa wala barua kuhusu kujiuzuru kwa mjumbe yeyote wa kamati anayoiongoza.

Chanzo:  MALUNDE 1 BLOG

 

Waandishi wa habari wakifuatilia hoja za mheshimiwa David Nkulila wakati wa kutangaza maamuzi hayo.

Mheshimiwa David Nkulila akielezea jambo wakati wa mkutano huo kwa wanahabari (Hawapo pichani).

 

Share:

Leave a reply