Dk. Arnold Kashembe ateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Simba SC

1506
0
Share:

Klabu ya Simba SC imetoa taarifa kuwa imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa Katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo, isome taarifa ya Simba hapa chini.

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iiliyokutana jana jioni,kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam,imemteua *Dr Arnold Kashembe* kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu. 

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja. 

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.

Share:

Leave a reply