Dk. Kigwangalla aendelea kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la Nzega Vijijini kwa kumchagua

249
0
Share:

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla ameendelea Vijiji mbalimbali vya Kata za Jimbo hilo lengo la kuwashukuru Wananchi hao kwa hatua yao ya kumchagua.

Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu,  Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19.

Katika ziara hiyo, Dk. Kigwangalla amewashukuru wananchi hao huku akiwataka kuendelea kuwa na Imani nae pamoja na Serikali iliyopp madarakani kwani imejipanga kuwaletea maendeleo wananchi wote.

“Kwanza nashukuru kwa kura zenu. Hakika zilitosha kuniwezesha mimi kuwa Mbunge. Kwa kura zenu  nyingi pia zimewezesha kumpata Rais wetu Dk. Magufuli na Diwani wetu. Nawashukuru sana Wana Nzega Vijijini” alieleza Dk. Kigwangalla.

Aidha, Dk. Kigwangalla pia aliweza kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi hao ikiwemo vijana ambayo hapo awali aliwaahidi.

Kata zinazounda Jimbo hilo la Nzega Vijijini ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.DSC_1796

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitia saiani wakati wa mkutano wa Kata ya Puge

DSC_1576

Kundi la Wazee wa mila wa Waswezi wakitoa burudani

DSC_1513

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wazee wa mila wa Waswezi wa Kata ya Nkiniziwa

Share:

Leave a reply