Dk. Kigwangalla afanya ziara ya kustukiza Hospitali ya Rufaa ya Kitete, Tabora atoa maagizo mazito

629
0
Share:

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla  amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo Mkoani Tabora na kutoa siku Saba kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya kumaliza changamoto za mradi wa ujenzi wa Theatre na Chuo cha AMO.

“Nimefanya ziara hii ya kushtukiza katika Hospitali hii ya Rufaa ya Kitete ili kujionea miradi ya Theatre (chumba cha upasuaji) na mradi wa Chuo Cha AMOs.   Hii ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo niliyoyatoa Mwaka mmoja uliopita. Nimesikitika kukuta hali iko vile vile na nimeagiza Katibu Mkuu Afya afike ndani ya siku saba atatue mkwamo huu na anipe taarifa.” ameeleza Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameongeza kuwa,  Theatre  na Chuo vimekamilika na vina hadi samani ndani toka miaka zaidi ya miwili iliyopita. Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part funding, huku Benki ya Maendeleo ya Africa ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia moja hivyo amemtaka Katibu Mkuu wa Afya kufika haraka na apatiwe majibu kwa ajili ya kuchukua maamuzi kwa waliozembea.

Akihitimisha ziara yake, amesema,  Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa amefurahishwa  kukuta maagizo kama kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za wanawake wajawazito na watoto na kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote muhimu na huduma kwa wateja kwa maana ya lugha nzuri ya wahudumu yametekelezwa kwa mafanikio makubwa.

“Wamefanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa na sasa hakuna tena msongamano nawapongeza kwa kuchukua hatua za haraka katika hili baada ya kutoa maagizo hivyo nitaendelea kupitia tena siku yoyote kuona utekelezaji huu kama utaendelea ama ni  wa muda,” alimalizia Dk. Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla akiwa kakatika Hospitali ya Kitete, Tabora ma baadhi ya viongozi wa Hospitali hiyo wakati wa ziara hiyo leo 27 Januari 2017 

Share:

Leave a reply