Dk. Kigwangalla ahitimisha ziara mkoani Ruvuma, atoa maagizo ya kuboresha huduma za afya

449
0
Share:
Naibu waziri wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Dk. Hamisi Kigwangalla amehitiisha ziara yake ya siku nne mkoani Ruvuma katika ziara yake ya kikazi kukagua huduma za Afya na kutoa maagizo mbalimbali ya uboreshaji huduma.
Katika ziara yake hiyo, iliyoanzia Wilaya za Tunduru, Namtumbo, Mbinga, Nyasa, Wilaya ya Songea Mjini na Halmashauri ya Madaba ambapo kote huko alikutana na changamoto mbalimbali za utoaji wa huduma hizo za Afya huku kubwa likiwa uhaba wa vyumba vya Upasuaji (Theater ),  ukosefu wa vifaa tiba pamoja na wahudumu kutozingatia suala la usafi.
Dk. Kigwangalla amewaagiza Wakurugenzi wote wa Mkoa huo kuhakikisha wanasimamia ipasavyo bajeti za huduma za Afya kwenye vikao vyao kwa kutoa vipaumbele ili kusaidia wananchi wao.
Akiwa katika ziara  ya kikazi ya ukagazi wa utekelezajiwa agizo la uboreshaji wa vituo vya afya katika kila Kata nchini lilitolewa Desemba 2016, Dk. Kigwangalla  katika ziara yake Wilaya ya Mbinga aliweza kutembelea kituo cha Afya Kalembo na Hospitali ya Wilaya ya Mbinga ambapo alijionea mambo mbalimbali  na kutoa maagizo kwa uongozi wa Wilaya hiyo ikiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanaboresha mapungufu yaliyopo.
“Munatakiwa kufanya marekebisho ya miundombinu ili huduma zitolewazo na kituo cha afya cha Kalembo  kwani hakina huduma bora licha ya kuanza  muda mrefu. Mulitakiwa muwe na Chumba cha Upasuaji, Maabara yenye kukidhi vigezo vya kupima magonjwa mbalimbali,” alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa upande wa Hospitali ya Wilaya aliagiza wahakikishe wanafanya maboresho katika maeneo yao mbalimbali ikiwemo kutengeneza vifaa vya uchunguzi na masuala mengine ya kitalaam ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi wa kada hiyo ya Afya ndani ya Wilaya ya Mbinga.
Kwa upande wa ziara yake hiyo Wilaya ya Nyasa, Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea kituo cha Afya Mbamba Bay ambapo pia aliweza kwenda kushuhudia eneo litakalojengwa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa.
Aidha, akikagua Kituo hicho cha Afya cha Mbamba Bay, aliweza kufanya mkutano na wananchi ambao pia wilitoa maoni yao  juu ya uboreshaji wa huduma hizo za Afya.
Hitimisho ya ziara hiyo hiyo ilimalizikia kwenye kituo cha Afya Mji  kilichopo Songea Mjini na baadae kituo cha Afya Madaba kilichopo Songea vijijini ambapo aliagiza wahakikishe wafanyia maaboresho haraka  chumba cha upasuaji.
Share:

Leave a reply